Kwa mujibu wa tovuti ya People mwanamke huyo amefungua kesi hiyo katika Mahakama ya Haki huko Kaunti ya Clark, Nevada, akidai kuwa yeye hakuwa na kosa lolote bali msanii huyo ndio aliomba amwagiwe maji.
“Alijitokeza jukwaani katika hali ya joto kali, na alipokuwa ameshika kipaza sauti, alitoa ombi kwa mashabiki wamwagie maji,” amesema
Kesi hiyo inadai kuwa Cardi alitoa ishara na kauli mara kwa mara zinazohamasisha mashabiki waliokuwepo kwenye tamasha kumwagia maji huku akitoa ruhusa ya kumwagia na vinywaji vingine. Hata hivyo, haijafahamika wazi kuwa video inayoonesha tukio hilo ilirekodiwa kabla au baada ya tukio hilo.

Doe anadai kwamba Cardi alifanya kitendo hicho kwa kukusudia hivyo basi anamshtaki kwa kosa la shambulio la kukusudia (assault) pamoja na kumpiga (battery) ambapo alidai kuwa alikumbwa na mshtuko mkubwa wa kihisia, fedheha, aibu na majeraha ya kimwili. Lakini pia anaishitaki kampuni ya Drai’s Management Group kwa uzembe na kutochukua hatua kwa msanii huyo.
Ikumbukwe kuwa kipaza sauti hicho kilichotumika katika tukio hilo kilipigwa mnada na kuuzwa kwa takribani dola 99,000 na Scott Fisher, mmiliki wa The Wave, jambo ambalo Doe anadai lilimpa msogo wa mawazo na kihisia.
Aidha dhumuni la kufungua kesi hiyo ni kudai fidia ya kawaida pamoja na fidia ya adhabu (punitive damages). Aidha kwa mujibu wa Drew Findling, wakili wa Card ameeleza kuwa awali kesi hiyo ilifutwa lakini mwanamke huyo ameamua kuirudisha tena kwa lengo la kujipatia pesa.
Leave a Reply