Wanandoa ambao harusi yao ilitikisa Tanzania, Nigeria na mataifa mengine Jux na mkewe Pricy wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.

Kupitia ukurasa wa instagram wa wanandoa hao wameshare picha za mrembo huyo zikimuonesha ni mjamzito ambaye anatarajia kupokea mtoto wake wa kwanza hivi karibuni.
Jux alifunga ndoa na Priscyla Februari 7, 2025, jijini Dar es Salaam, Aprili 2025, wanandoa hao walisafiri hadi Nigeria kwa ajili ya sherehe ya kitamaduni mjini Lagos Aprili 17, iliyofuatiwa na harusi ya kanisani Aprili 19.

Walihitimisha sherehe hizo kwa tafrija kubwa iliyofanyika Tanzania Mei 28 huku sherehe hizo zikiiteka mitandao ya kijamii.
Leave a Reply