Shatta Wale adiwa kususia pesa kisa Diamond

Shatta Wale adiwa kususia pesa kisa Diamond

Msanii tokea nchini Ghana, Shatta Wale anadaiwa kurudisha kiasi cha pesa alicholipwa kwenye show kisa kupewa pesa ndogo ukilinganisha na wasanii wengine kama Diamond na Davido

Show hiyo ambayo ilifanyika Jumamosi ya Machi 22, 2025, huko nchini Ghana ilikuwa ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya bilionea 'Richard Nii-Armah Quaye'. Ambapo aliwaalika wasanii wakubwa barani Afrika wakiwemo Diamond Platnumz, Davido, Sarkodie, Shatawale na wengine.

Inaelezwa kuwa Shatta Wale amesusia dola 200,000 sawa na Sh532 milioni ambayo alilipwa kwenye show hiyo ukilinganisha na pesa walizolipwa Diamond na Davido ambao walilipwa (dola 600k & 500k sawa na Sh1.6 Bilioni na Sh1.3 Bilion).

Shatta Wale anaamini kuwa yeye na Sarkodie kama wasanii wazawa wa Ghana walitakiwa kulipwa vizuri zaidi ya wasanii wageni ila kilichofanyika ni kama kuwadharau.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags