Nay Amlipua Billnass, Adai Ni Mwizi

Nay Amlipua Billnass, Adai Ni Mwizi

Wakati rapa na msani wa Bongo Fleva, Billnass akifanya mahojiana leo na moja ya chombo cha habari nchini, aliulizwa changamoto gani iliyopelekea kumzuia mke wake mwanamuziki, Nandy kushirikishwa kwenye albamu ya Rais wa Kitaa ya kwake Nay Wamitego.

Nenga amesema kwamba Nay alitaka afungwe jela hivyo ameendelea kujifungia ikiwa ni pamoja na kumzuia mke wake Nandy kushirikiana na Nay.

"Hamna hata shida kubwa kwa sababu wakati inatokea alitamani mimi niende jela, kwahiyo mimi bado nipo jela nimejifungia kule ambapo alitaka niwepo, sijafanikiwa kwenda jela alipotaka lakini bado nipo alipotaka kimaono" amesema Billnass

Hata hivyo, Nay amemjibu Nenga kupitia upande wa comment wa chapisho hilo akisema Nenga ni mwizi na angeenda jela kwa tabia yake hiyo.



"Msanii mjinga ambae amekua anapenda trending kwa style yoyote ile aya acha nikupe unachotaka wewe ni mwizi ungeenda jela kwa tabia yako ya wizi. Nina kazi nyingi za kufanya nianze kukukandamiza wewe kwenda jela how yani.?! Mgande Nandy ivyo ivyo ili usije ukaendelea na udokozi.!!" ameandika Nay






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags