Kawaida kwenye kiwanda cha burudani mashabiki hudhani maisha ya mastaa wanaowashabikia yapo mikononi mwao, yaani hutaka kufahamu kila kinachowatokea mastaa hao. Kuanzia maisha yao binafsi hadi kazi wanazotoa.
Licha ya kuwa wapo wanaoweka wazi kila hatua ya maisha yao. Lakini wapo wanaoyaweka faragha hasa linapokuja suala la mahusiano. Hawa hapa wasanii waliowahi kufunga ndoa kwa siri.
Kanye West na Bianca Censori
Mwanamuziki maarufu Kanye West alifunga ndoa na mrembo Bianca Censori Desemba 2022, baada ya talaka yake na Kim Kardashian. Wawili hao walifanya sherehe ya kimya kimya yaani kwa siri.
Hivyo basi ndoa ya wawili hao ilifichuka rasmi Oktoba 2023, wakati ilipothibitishwa kuwa walifunga ndoa kwa siri. Hii ilijulikana baada ya kutolewa kwa nyaraka rasmi za ndoa kutoka California, zikionyesha kuwa walipata leseni ya ndoa ya siri.
Kabla ya kuthibitishwa kwa ndoa yao, Kanye na Bianca walikuwa wakionekana pamoja mara kwa mara katika matukio ya umma, lakini hawakuthibitisha hadharani uhusiano wao.
Baada ya ndoa yao, walikuwa na wakati mgumu katika uhusiano wao, ikiwa ni pamoja na uvumi wa kupeana talaka. Hata hivyo.
Justin Bieber na Hailey Baldwin
Justin Bieber na Hailey Baldwin walifunga ndoa kwa siri mnamo Septemba 2018, miezi miwili baada ya kuvishana pete ya uchumba . Walifunga ndoa katika jiji la New York, na baadaye walifanya sherehe ya kidini kwa familia na marafiki.
Ndoa ya wawili hao ilifichuka, wakati walipoonekana wakitembea pamoja kuelekea jumba la mahakama huko New York City, ambapo walipata leseni ya ndoa. Hata hivyo, Hailey Baldwin alikanusha taarifa hizo kupitia mtandao wa Twitter, akisema: "Ninaelewa wapi uvumi unavyotokea, lakini bado sijaolewa,"
Baada ya siku moja, Justin Bieber alithibitisha ndoa hiyo kwa kuandika ujumbe wa kimapenzi kwenye Instagram, akisema: "Niko tayari kutumia maisha yangu kujua kila sehemu yako, kukupenda kwa uvumilivu na kwa upole.
Ndoa rasmi ya kidini ilifanyika baadaye Septemba 30, 2019, huko Bluffton, South Carolina, ambapo walifanya sherehe kubwa kwa familia na marafiki.
Beyoncé na Jay-Z
Beyoncé na Jay-Z walifunga ndoa kwa siri mnamo Aprili 4, 2008, katika sherehe ya kifahari iliyohudhuriwa na familia na marafiki wachache. Sherehe hiyo ilifanyika katika jumba la kifahari la Jay-Z huko New York.
Katika ndoa hiyo ilikuwa na sherehe ya faragha iliyohudhuriwa na wageni 40 pekee, wakiwemo familia zao na marafiki wa karibu. Kwa kuwa walikuwa na mapenzi makubwa namba 4 Beyoncé alizaliwa Septemba 4, Jay-Z alizaliwa Desemba 4, na walifunga ndoa Aprili 4 walichagua tarehe hii kama kumbukumbu muhimu katika maisha yao .
Ingawa ndoa yao ilifichuka Aprili 2008, Beyoncé alithibitisha rasmi ndoa hiyo miezi sita baadaye, Oktoba 2s 008, alipozungumza na jarida la Essence. Katika mahojiano hayo, alisema: “ Alikataa pete ya uchumba kwa sababu aliona kuwa watu wanaweka umuhimu mkubwa kwenye hilo, na badala yake alichagua kuvaa pete ya ndoa yenye alama ya namba IV (4) kama ishara ya upendo wao .

Leave a Reply