Baada ya kufanya balaa kubwa nchini Tanzania katika harusi yao na sasa kumeanza kuchangamka nchini Nigeria kufuatia na muendelezo wa shughuli ya mwanamuziki Jux na mpenzi wake mwigizaji ambaye ni mzaliwa wa Nigeria, Priscilla.
Shamra shamra hizo ni mwanzo wa harusi ya kitamaduni itakayofanyika siku chache zijazo ambapo imeeanza usiku wa kuamkia leo leo Aprili 14, 2025 ambapo mwanadada huyo alifanyiwa ‘Bridal shower’ iliyohudhuriwa na marafiki pamoja na watu wake wa karibu.
Jux na Priscilla wanatarajia kufanya harusi ya kitamaduni April 17, 2025 jijini Lagos huku ikitajwa kuwa moja ya matukio makubwa yatakayofanyika nchini humo mwezi huu.
Wawili hao walifunga ndoa Februari 7,2025 ndoa ambayo ilihudhuriwa na na watu wachache wakiwemo ndugu wa karibu pamoja na wasanii kama vile Diamond Platnumz, Zuchu, S2kizzy, Abba, Ommy Dimpoz na wengine.
Mahusiano ya wawili hao yalianza mapema Agosti 2024 huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandano ya kijamii ya ndani na nje ya Tanzania baada ya Jux kwenda ukweni nchini Nigeria.
Ikumbukwe kabla ya Jux kuwa kwenye mahusiano na Priscilla, alikuwa na Karen Bujulu. Priscilla Ajoke Ojo alionekana kwa mara ya kwanza na Jux July 19,2024 kwenye moja ya kumbi za starehe zilizopo jijini Dar es salaam. Na hii inakuwa ndoa ya kwanza kwa wapenzi hao wawili.

Leave a Reply