Kazi ya yai katika uboreshaji wa ngozi na nywele

Kazi ya yai katika uboreshaji wa ngozi na nywele

Oooooooh! Kama kawaida yetu ni Ijumaa nyingine watu wangu wanguvu, harafu ni kama weekend inakuja kwa kasi mana mambo mengi muda mchache, basi bwana week hii katika fashion tumekusogezea mada ambayo itakusaidia katika kuboresha na kukupatia muonekano mzuri wa ngozi yako. 

Kawaida yai limekuwa na matumizi kama chakula kwa muda mrefu, wapo ambao hutumia chakula hicho kwa kukaanga, kuchemsha, kunywa likiwa bichi au kuchanganya katika vyakula vingine mbalimbali.

Lakini pia kuna matumizi ya yai zaidi ya chakula, kwani linauwezo mkubwa wa kurutubisha ngozi, nywele na pia kuondoa uchovu na kuondoa dotidoti katika uso.

Jinsi ya kufanya


Ukitaka kutumia yai kuboresha muonekano wa ngozi na nywele zako,
chukua yai, changanya na asali kijiko kimoja cha chai,  mafuta ya olive halafu chukua mchanganyiko huo kisha pakaa usoni na shingoni  na katika nywele, paka kwenye nywele halafu vaa mfuko kichwani kisha kaa nao kwa dakika 10 hadi 15, hii itasaidia kama una mashimo usoni yatokanayo na chunusi yataweza kupotea na kwenye nywele zako itakusaidia kuondoa miwasho sugu na inasaidia zisikatike pindi unapo zichana.

Hii sio tu inaondoa makovu pia itasaidia kulainisha ngozi yako na kuwa nyororo, mchanganyiko huu pia utasaidia kukuondolea michubuko au alama za kuungua na jua, mafuta au krimu usoni. Haswa wale wenzangu na mie ambao wanaweusi chini ya macho itakusaidia 100%.

Pia unaweza kutenganisha kiini cha yai na ule ute mweupe, kisha chukua ute weka kwenye kikombe au bakuli, baada ya  hapo pigapiga ule ute  hadi uwe na mapovu kisha chukua povu,  linawe usoni au paka mwili mzima kisha liache likauke.

Baada ya hapo osha uso au mwili wako na maji ya uvuguvugu, ukifanya hivyo mara kwa mara itakusaidia kufanya ngozi yako iwe anga’avu.

Na sio katika kukupatia muonekano bora tuu bali pia huondoa uchovu, mfano umetoka kazini na  umechoka na unataka kutoka usiku kwenda kwenye party au shughuli yoyote basi yai pia linaweza kukusaidia kukufanya ukawa mtu mwenye nguvu.

Chakufanya chukua ute wa yai na pakaa chini ya jicho na uache kwa dakika 10 hadi 15 kisha safisha, itasaidia kuondoa muonekano wa uchovu katika macho yako na itakusaidia kukupatia muonekano wa ukakamavu.

Yai sio tuu inasaidia kukupatia muonekano bora lakini pia linaweza kuwa tiba kwako, Kama unawashwa mwili mzima bila sababu yoyote yaani hujala chakula cha kukudhuru inatokea tu mwili unakuwa unawasha na kutoka ukurutu mdogomdogo. 

Chukua ute wa yai kidogo halafu nyunyiza katika maji utakayoyaoga sambamba na sabuni ya kuogea, ndani ya siku chache utaona matokeo mazuri kwenye rangi ya ngozi yako na muonekano wako kwa ujumla.

Sasa hii ni babu kubwa, nikikwambia yai lina maajabu yake katika kubadilisha mwili wako basi namaanisha ninacho kizungumza. Ute wa yai pia unasaidia kuondoa makovu ukiwa unatumia kwa muda mrefu itakupa matokeo mazuri.

Kama una kovu la muda mrefu, cha kufanya inabidi uwe na ute wa yai ya tango, chukua tango lako liblend na maganda yake kisha changanya na ute wa yai, kisha paka katika kovu lako, hii husaidia kulainisha makovu na unapotumia kwa muda mrefu huondoa makovu pia.

Nyie nyie, hii nondo ya leo asiesoma atakuwa amepitwa haswa maana ni bonge la mada ambayo imegusa katika kila sekta kwenye nywele na ngozi yako. Ebu pita katika page zetu @Mwananchiscoop na utueleze yai limekusaidia vipi katika kuboresha muonekano wako.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags