Manara awagumzo mitandaoni

Manara awagumzo mitandaoni

Moja kati ya story inayobamba katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni ya aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara kutambulishwa rasmi kujiunga na klabu ya Yanga.

Manara amejiunga na klabu hiyo ya Yanga jana Agosti 24, 2021 na uamuzi huo aliutangaza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Manara alisema amejiunga na klabu kubwa kuliko zote Afrika mashariki na kati, hivyo lazima yeye afanye kazi na watu wakubwa na kuongeza kuwa atashirikiana na wenzake kutimiza malengo ya klabu.

Hata kupitia ukurasa wake wa Instagram Manara aliandika kuwa “Mja wa stara hadhaliliki, wananchi nawaahidi utumishi mkubwa na nitapigania hii club kwa nguvu kubwa Insha’Allah, wanasimba kabla ya kunilaumu mimi jiulizeni nyie mngekuwa mimi mngefanyaje? mabosi zenu hawakunitaka nifanye nini? Alihoji Manara

Hata hivyo baada ya kauli huyo baadhi ya mashabiki wa Simba walimshukia na kumuita msaliti na kusema ni heri alivyoondoka katika timu hiyo.

Ila hali ni tofauti kwa mashabiki wa Yanga ambao wengi wameonesha kufurahishwa na kitendo cha Manara na kumkaribisha

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags