Jarida la Forbes limetoa orodha ya wasanii bora wa hip-hop wa muda wote huku jina la Kendrick likitokea kama msanii wa pili kwenye orodha hiyo.
Orodha hiyo ambayo ilikuwa imeshiba majina ya manguli wa hip-hop Kendrick ameonekana kupenya na kukaa juu yao huku orodha hiyo ikiongozwa na Jay Z ambaye ameshika nafasi ya kwanza.
Kendrick ambaye amekuwa na wakati mzuri kimuziki kwa mwaka 2024 amekaa mbele ya rapa wakubwa ambao walimtangulia kwenye muziki kama Lil Wayne, Tupac, J Cole, Kanye West n.k
Hata hivyo Kendrick anaheshimiwa kama mfalme wa muziki wa hip-hop wa kizazi cha sasa kutokana na ushawishi alionao kwenye kazi zake ambapo mwezi uliopita aliachia album kwa kushitukiza lakini bado akachukua vichwa vya habari na kushika nafsi ya kwanza kwenye majukwaa ya kidijitali zaidi ya 100 duniani.
Leave a Reply